Kanisa Katoliki nchini Zambia kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa kwa pamoja wamehitimisha Siku ya kimissionari duniani, kwa kutafakari uzoefu, mang'amuzi na utume wao wa kimissionari, tangu Wamissionari wa kwanza walipotia nanga nchini Zambia, yapata miaka mia moja na kumi na tisa iliyopita. Ilikuwa ni nafasi nyingine tena ya kutathmini hali halisi na changamoto wanazokabiliana nazo katika utangazaji wa Habari Njema ya Wokovu nchini Zambia.
Kanisa Katoliki Zambia linatambua kwamba asili yake ni umissionari, changamoto ni kuendelea kuadhimisha na kumwilisha uweli huu katika hali halisi ya maisha na utume wa Kanisa nchini humo mintarafu mwanga na changamoto zilizotolewa na Mababa wa Awamu ya Pili ya Sinodi ya Maaskofu wa Afrika.
Wakristo wote wanakumbushwa kwamba, kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo wanashiriki ule ukuhani, unabii na ufalme wa Kristo na hivyo wanatumwa ulimwenguni kote kutangaza Habari Njema ya Wokovu kwa njia ya ushuhuda wa maisha yao, wakiendelea kujenga mshikamano wa dhati kati yao kama Kanisa.
Ni matumaini ya Kanisa Katoliki Zambia kwamba, Kongamano la Kimissionari lililofanyika nchini humo kuanzia tarehe 13 hadi 16 Oktoba, 2010 litaendelea kuwa ni changamoto kwa Taifa la Mungu kujitambua kwamba, kila mmoja wao ni mmissionari na anatumwa kutangaza kweli za Kiinjili kwa njia ya ushuhuda wa maisha yake, wakipania kujenga umoja na mshikamano wa kikanisa kwa kushirikiana na wadau wengine kutoka sehemu mbali mbali za dunia.
Kila mwamini anaalikwa kushiriki utume na maisha ya Kanisa kwa ukamilifu zaidi, kadiri ya nafasi na vipaji vyake, kuendeleza kazi ya Uinjilishaji wa kina inayogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili, kwanza kabisa kwa kutambua na kuthamini ukristo wao na kama waamini wa Kanisa Katoliki, ili waweze kuwa kweli ni mashahidi amini wa kweli za kiinjili, bila kupindisha ukweli huo.
Wanapaswa kutambua kwamba, wao ni Taifa na Familia ya Mungu inayowajibika, mwaliko wa kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa mahalia, huku wakiendelea kusoma alama za nyakati, kwa kuangalia mabadiliko ya mwelekeo wa kidini na vipaumbele vyake katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii bila kusahau dhana ya utamadunisho, ili kweli tunu msingi za maisha ya kiafrika ziweze kumwilishwa katika maisha ya kikristo mintarafu mwanga wa Kiinjili.
Zambia kama lilivyo Bara la Afrika ina kiu ya Uinjilishaji wa kina, kwa kuendelea kuimarisha Jumuiya Ndogo ndogo za Kikristo; majadiliano ya kidini na kiekumene; kwa kukuza ushirikiano wa karibu zaidi na vyombo vya mawasiliano ya jamii vinavyopaswa pia kuinjilishwa na kuwa ni sauti ya wanyonge zaidi katika Jamii. Taasisi, vyuo na shule zinazomilikiwa na kuendeshwa na Mama Kanisa nchini Zambia, ziwe pia ni mahali pa uinjilishaji na mshikamano wa kidigu.
Kwa miaka mingi Zambia imepokea wamissionari kutoka nje, umefika kwa Kanisa la Zambia kuchangamkia utume wa kimissionari ndani na nje ya Zambia kadiri ya mahitaji ya Kanisa la Afrika na Ulimwengu kwa ujumla. Ili kufanikisha azma hii, lazima wajenge ile dhana ya kupatikana pamoja na kuendelea kukuza na kuimarisha miito mitakatifu ndani ya Kanisa. Source: Radio Vatican

No comments:
Post a Comment