Kardinali Marc Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu ndiye atakayeongoza jopo la viongozi wakuu kutoka Vatican wanaotarajiwa kuzindua rasmi hati ya kichungaji kutoka kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, baada ya Maadhimisho ya Sinodi ya kumi na mbili ya Maaskofu iliyofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 5 hadi 26 Oktoba, 2008; kwa kuongozwa na tema "Neno la Mungu katika maisha na utume wa Kanisa", hapo tarehe 11 Novemba, 2010..
Ujumbe wa kichungaji baada ya Sinodi umepewa jina kwa lugha ya Kilatini "Verbum Domini", Yaani "Neno la Bwana". Baadhi ya viongozi wanatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa hati hii ya kichungaji mara baada ya Sinodi ni pamoja na Kardinali Mteule, Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni; Askofu Nikola Eterovic, Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu pamoja na Monsinyo Fortunato Frezza, katibu mkuu msaidizi, Sinodi ya Maaskofu. Source: Radio Vatican

No comments:
Post a Comment