Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameunda jimbo Jipya la Bunda, kwa kumega baadhi ya maeneo ya Jimbo kuu la Mwanza na Jimbo la Musoma. Kwa heshima na tahadhima amemteua Mheshimiwa sana Padre Renatus Leonard Nkwande, aliyekuwa msimamizi wa Jimbo kuu la Mwanza, kuwa Askofu Mpya wa Jimbo la Bunda, Mara, Tanzania
Jimbo la Bunda, linaundwa na Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara na Wilaya ya Ukerewe inayovijumuisha visiwa vya Ukara, toka Mkoa wa Mwanza. Parokia ya Saragana na Mabui zinaunda sasa Jimbo Jipya la Bunda. Mpaka kati ya Jimbo la Musoma na Jimbo Jipya la Bunda ni Mto Suguti. Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Paulo, litakuwa ni Kanisa kuu la Jimbo Jipya la Bunda.
Askofu mteule Renatus Leonard Nkwande, alizaliwa kunako tarehe 12 Novemba, 1965, Parokia ya Sumve, Jimbo kuu la Mwanza. Alipata masomo yake ya sekondari, Seminari ya Makoko, Musoma na Nyegezi, Jimbo kuu la Mwanza.
Kunako Mwaka 1987 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho, Moshi, kwa ajili ya masomo ya Falsafa na baadaye mwaka 1989 aliendelea na masomo ya Taalimungu Seminari kuu ya Segerea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam. Alipadrishwa kunako tarehe 2 Julai 1995 akawa ni Padre wa Jimbo kuu la Mwanza.
Tangu alipopadrishwa amefanya shughuli mbali mbali za kichungaji kama Paroko msaidizi, Gombera wa Seminari ndogo ya Nyegezi, Jimbo kuu la Mwanza na baadaye kunako mwaka 2002 hadi 2005 alikwenda Roma kwa masomo ya Sheria za Kanisa, kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana.
Tangu mwaka 2008 hadi 2009 alikuwa ni Makamu wa Askofu, Jimbo kuu la Mwanza. Na baadaye mwaka 2009 aliteuliwa kuwa msimamizi wa Jimbo kuu la Mwanza kufuatia kifo cha Askofu mkuu Anthony Mayala.

Source: Radio Vatican
No comments:
Post a Comment