Jumapili ya kwanza ya kipindi cha Majilio inaufungua rasmi Mwaka Mpya wa Kanisa, hija ya maisha ya imani, inayowakumbusha waamini, Fumbo la Umwilisho na Siku ya ile ya mwisho, Yesu atakapokuja kuwahukumu wazima na wafu, kama waamini wanavyosali katika Kanuni ya Imani. Majilio linakuwa ni tukio la aina yake, kwani hapo mwili na roho vinaunganika kwa pamoja.
Hayo yamesemwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican, siku ya jumapili, tarehe 28 Novemba, 2010. Tukio la kungoja, linamshirikisha mwamini mmoja mmoja, familia na jamii kwa ujumla, katika hali na maisha ya kawaida kabisa. Maisha ya mwanadamu yanafumbatwa kimsingi katika fadhila ya matumaini, inayokuwa ni kipimo cha kimaadili na kiroho kwa kile anachotarajia na kutegemea katika maisha.
Baba Mtakatifu anawaalika waamini kila mmoja kujiuliza swali la msingi, katika kipindi hii cha Majilio, ni jambo gani analolitarajia katika maisha yake kama mtu binafasi, familia na taifa kwa ujumla. Kwa Waisraeli wakati wa Agano la Kale, walikuwa na tumaini kubwa la ujio wa Kristo, Masiha na Mteule wa Mungu, ambaye angekuja kuwakomboa watu kutoka katika utumwa wa kimaadili na kisiasa na hatimaye, kuanzisha Ufalme wa Mungu kati ya watu.
Hakuna mtu aliyefikiria kwamba, Masiha wa Bwana angeweza kuzaliwa na msichana kama Bikira Maria, mchumba wake Yosefu, mwenye haki. Hata ndani ya moyo wa Bikira Maria anasema Baba Mtakatifu, hakuwahi kufikiri hata kidogo, matumaini ya Ujio wa Masiha moyoni mwake, yalikuwa makubwa kutokana na imani na matumaini yake, hali iliyomfanya kustahilishwa kuwa ni Mama wa Mkombozi.
Mambo mengine anasema Baba Mtakatifu, Mwenyezi Mungu mwenyewe alikuwa ameyaandaa tangu kuumbwa kwa ulimwengu, ndiyo maana Bikira Maria alikuwa amejaa neema, mkweli na muwazi mintarafu mpango wa Mungu katika maisha yake, changamoto kwa waamini kumjifunza Bikira Maria katika maisha yao.
Bikira Maria ni mwanamke wa Kipindi cha Majilio, aliyejitahidi kulimwilisha tukio hili katika hali mbali mbali za maisha yake, kwa ari na mwelekeo mpya wa maisha, akiwa na kiu kubwa ya matumaini, inayozimwa na ujio wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.
Baba Mtakatifu anawakumbusha waamini kwamba, Kipindi cha Majilio kiwasaidie kujiandaa kwa makini, kwa ajili ya adhimisho la Fumbo la Umwilisho. Ni changamoto ya kuruhusu neema ya Mungu, maisha ya sala na toba, pamoja na matendo ya huruma, katika kipindi hiki cha Majilio, waamini wanapongojea kuzaliwa kwa Masiha. Ni mwaliko wa kusimama kidete kulinda na kutunza zawadi ya maisha, kama alivyofanya Bikira Maria.

Source: Radio Vatican